
BALEKE, MAYELE WAPEWE TU MAUA YAO
“WASHA Wifi na usizime Data, hawa ni Wekundu wa Msimbazi Simba, wanaendelea palepale walipoishia, Jean Baleke namna ambavyo anafanya, ndivyo ambavyo anaendeleza kwenye Dimba la Benjamin Mkapa,” alisikika akiunguruma mtangazaji wa kituo cha ZBC2, Ghalib Mzinga akisherehesha bao la Baleke dhidi ya Wydad Casablanca. Ndiyo, Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam…