
AZAM FC WAMEKWAMA KWA MARA NYINGINE TENA
KLABU bora Bongo Azam FC kwa mara nyingine tena wamekwama kufurukuta mbele ya Singida Fountain Gate katika Kombe la Mapinduzi kwa kuwa ni mara ya pili kufungashiwa virago na timu hiyo. Ikumbukwe kwamba Januari 8 2023 ubao wa Uwanja wa Amaan ulisoma Azam FC 1-4 Singida Fountain Gate katika hatua ya robo fainali zama hizo…