MUDA WA KAZI KWA TAIFA STARS NI SASA

    TIMU ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kwa sasa ipo kambini ikiwa ni maandalizi ya mwisho kwa ajili ya AFCON 2023 inayotarajiwa kufanyika Ivory Coast.

    Hii sio kazi rahisi kwa wachezaji kwa kuwa kila timu inahitaji matokeo ndani ya uwanja katika dakika 90. Kila mchezaji anajukumu la kuhakikisha kwamba anapambania kombe na kufanya vizuri kila akipata nafasi.

    Muda ni sasa kufanya maandalizi mazuri kwa ajili ya kupata matokeo chanya. Inawezekana kutokana na uwezo wa wachezaji ambao wameitwa kwenye timu ya taifa.

    Ukweli ni kwamba kila mchezaji ana nguvu kubwa kwenye kusaka matokeo na ushindi kupatikana. Ambacho kinatakiwa kwa sasa ni kuwa makini kufuata maelekezo ambayo yanatolewa.

    Wachezaji muda mfupi uliopo kwa ajili ya maandalizi utumike kwa umakini ili kuongeza furaha kwa Watanzania. Kushiriki AFCON na kupata matokeo mazuri ni jambo kubwa ambalo linapaswa kuandikwa kwenye vitabu vya kumbukumbu.

    Waliopewa jukumu hilo ni wachezaji waliopo kambini na mashabiki kuendelea kuwaombea wachezaji wafanye vizuri kwenye kila mechi ambazo watashuka uwanjani.

    Ipo wazi kuwa furaha ya mashabiki ipo kwenye matokeo mazuri na furaha ya wachezaji inabebwa na kupata ushindi ndani ya uwanja kwenye mchezo husika.

    Muda wenyewe ni sasa na wachezaji wanatambua kwamba inawezekana kwa kuwa kupitia mazoezi ambayo wanafanya wanakuwa imara kwa ushindani kitaifa na kimataifa.

    Nidhamu kubwa inahitajika wakati wa maandalizi hii itaongeza uelewa kwa wachezaji. Kufanya vizuri kwenye mazoezi kutaleta mwendelezo mzuri mpaka eneo la mechi ambayo ni kumalizia kazi iliyoanza kutengenezwa mwanzo uwanja wa mazoezi.

    Kila mmoja atimize majukumu yake kwa wakati na bila kusahau kwamba Watanzania wanawaamini kwenye kufanya kweli na kuwapa furaha baada ya ushindi.

    Inawezekana kupata ushindi kwenye mechi zote ikiwa wachezaji watajituma bila kuogopa na kupunguza makosa ndani ya uwanja huku wakitumia makosa ya wapinzani kupata ushindi.

    Inafahamika kwamba mchezo wa mpira ni mchezo wa makosa hivyo ni muhimu kwa wachezaji kupunguza makosa kila wakati na kuwa makini kutumia makosa ya wapinzani.

    Mashabiki wanapenda mpira na furaha yao itaongezeka matokeo yakiwa mazuri kwenye mechi zote ambazo wachezaji watakuwa uwanjani kusaka ushindi muda ni sasa kufanya kweli ndani ya uwanja.

    Maandalizi mazuri yatakuwa silaha bora kupata ushindi kwenye mechi hizo zijazo ambazo zote zitakuwa ngumu kwani hakuna timu ambayo haipendi kupata ushindi uwanjani.

    Benchi la ufundi pamoja na wachezaji ni muda wa kuongea lugha moja ya ushindi kuelekea kwenye mechi hizi ngumu kila mmoja anapaswa kutambua kwamba hakuna kinachoshindikana.

    Wale ambao wanahofu hawapaswi kuwa nayo bali waamini kwamba kazi inakwenda kufanyika. Wachezaji walioitwa kwenye timu ya taifa wana uwezo na wanatambua kwamba taifa linawategemea.

    Kuiwakilisha Tanzania kwenye jukumu kubwa la kitaifa ni muhimu kwa kila mchezaji kujitoa kwa hali na mali ili kuipeperusha bendera ya Tanzania kitaifa na kimataifa.

    Previous articleMBWANA SAMATTA: MISRI NI WAPINZANI WAZURI
    Next articleMchezo wa Kasino Mafia Clash, Kutana na Mwamba Anayelipa Zaidi