MORRISON NDANI YA SIMBA NI 500

KIUNGO wa Simba, Bernard Morrison kwa msimu wa 2021/22 ndani ya kikosi cha Simba ameyeyusha dakika 500 katika mechi za Ligi Kuu Bara. Simba ikiwa imecheza jumla ya mechi 15 ambazo ni dakika 1,350 alikosekana katika dakika 850 uwanjani. Kabla ya kusimamishwa kutokana na kile kilichoelezwa kwamba ni utovu wa nidhamu mechi yake ya mwisho…

Read More

CHAMA ATUPIA SIMBA IKISHINDA MBELE YA MBEYA KWANZA

CLATOUS Chama,mwamba wa Lusaka ametupia bao pekee la ushindi mbele ya Mbeya Kwanza katika mchezo wa Ligi Kuu Bara. Ni bao la kwanza kwa Chama akipachika bao hilo akitokea benchi alipokuwa akisoma mchezo. Ni dakika ya 85 mpira ulijazwa kimiani na kufanya mashabiki wa Simba kunyanyuka jukwaani. Unakuwa mchezo wa pili kwa Simba kushinda bao…

Read More

AZAM FCHESABU ZAKE ZIPO NAMNA HII

UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi kuwa malengo yao makubwa msimu huu ni kuhakikisha wanashinda michezo mingi kadiri inavyowezekana ili kujiweka kwenye nafasi nzuri katika msimamo na kukata tiketi ya kucheza mashindano ya kimataifa msimu ujao. Azam ambayo ipo chini ya kocha Abdi Hamid Moallin, ipo nafasi ya tatu na pointi zake ni 24 kibindoni….

Read More

KOCHA TANZANIA PRISONS:PENALTI YA SIMBA NI HALALI

SHABAN Kazumba, Kocha Msaidizi wa Tanzania Prisons, amesema kuwa bao la penalti ambayo walipata Simba  ni halali kwa kuwa ilitolewa na mwamuzi kutokana na makosa ambayo walifanya. Bao hilo lilifungwa na Meddie Kagere na lilionekana kuwa na utata kutokana na wachezaji wa Prisons kumfuata mwamuzi kulalamika juu ya penalti hiyo. Kazumba aliliambia Championi Jumamosi kuwa:-“Simba…

Read More

HII HAPA RATIBA YA LEO BONGO

LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea kwa mara nyingine tena leo Februari 6 2022 ikiwa ni mzunguko wa 14. Timu tatu zitakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu kwenye mechi ambazo watacheza katika uwanja Ni Geita Gold v Polisi Tanzania Uwanja wa Nyankumbu. Namungo v Mtibwa Sugar, Uwanja wa Majaliwa. Simba v Mbeya Kwanza, Uwanja wa…

Read More

SIMBA YATAJA NAMNA ITAKAVYOTWAA UBINGWA WA LIGI

PABLO Franco, Kocha Mkuu wa Simba ameweka wazi kuwa mbinu pekee ya timu hiyo kutwaa ubingwa msimu huu na kuwafunika wapinzani wao Yanga ni kushinda mechi ambazo watacheza. Simba ni mabingwa watetezi, wanapambana kufikia malengo yao wakiwa wamejichimbia nafasi ya pili na pointi 28 huku wakiwa wamepoteza mechi mbili kati ya 14.  Pablo amesema kuwa…

Read More

TANZANITE WAREJEA DAR SALAMA WAKITOKEA ETHIOPIA

TIMU ya taifa ya Wanawake chini ya miaka 20, Tanzanite Queens leo Februari 5 imerejea salama Tanzania ikitokea nchini Ethiopia ambapo ilikuwa na kazi ya kuipeperusha bendera  kwenye mashindano ya kimataifa. Jana ilikuwa kwenye mchezo wa pili dhidi ya Ethiopia baada ya ule wa awali uliochezwa Uwanja wa Amaan ubao kusoma Tanzanite 1-0 Ethiopia na…

Read More

JUKUMU LA PETER BANDA HILI HAPA

SIMBA imeweka wazi kuwa mara baada ya kiungo mshambuliaji wao, Peter Banda kurejea nchini akitokea Cameroon alipokuwa na kibarua cha kuiwakilisha Malawi kwenye mashindano ya Afcon, moja kwa moja atajiunga na programu za maandalizi ya michezo ijayo hususani mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast. Katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Simba imepangwa kwenye Kundi D pamoja na timu za…

Read More

MORRISON ATAJWA KUIBUKIA YANGA

KIUNGO mshambuliaji wa Kimataifa raia wa Ghana, anayekipiga ndani ya Klabu ya Simba, Bernard Morrison amemamisha kwa muda hadi suala lake la kinidhamu litakapo patiwa ufumbuzi. Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya klabu hiyo, Morrison amekuwa na tabia ya kutoka kambini bila ruhusa kinyume na taratibu Aidha ametakiwa kutoa maelezo ya maandishi kwa Mtendaji Mkuu…

Read More

NDEMLA MAMBO MAGUMU MTIBWA SUGAR

KIUNGO wa Mtibwa Sugar, Said Ndemla mambo kwake yamekuwa magumu ndani ya Mtibwa Sugar kwa sasa kwa kwa tangu alipofunga bao Desemba 12/2021 mpaka leo hajaweza kufurukuta tena kwa kufunga wala kutoa pasi ya bao. Ndemla upo hapo kwa mkopo ambapo alijiunga na timu hiyo akitokea kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Pablo Franco….

Read More

SIMBA QUEENS YAPIGA KIFURUSHI CHA WIKI

SIMBA Queens imesepa na ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya JKT Queens katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Mo Simba Arena uliopo Bunju. Miongoni mwa waliotupja ni pamoja na Joel Bukulu ambaye alitupia bao moja kwa mkwaju wa penalti. Pia Opa Clement alitupia mabao mawili katika mchezo wa leo na anafikisha mabao 17 kibindoni. JKT Queens…

Read More

SIMBA QUEENS KUVAANA NA JKT QUEENS LEO

SIMBA Queens leo Februari 4 inatarajiwa kuwa na mchezo wa kusaka pointi tatu mbele ya JKT Tanzania. Huu ni mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Bunju Complex. Ni saa 10:00 jioni mchezo unatarajiwa kuchezwa kwa kila timu kusaka pointi tatu muhimu. Simba Queens mchezo wake uliopita ilikuwa dhidi ya Mlandizi Queens…

Read More