BANDA ASHINDA TUZO YA MCHEZAJI BORA
KIUNGO wa Simba, Peter Banda ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashabiki kwa mwezi Machi. Banda ameweza kushinda tuzo hiyo akiwazidi kura nyota wawili ambao aliingia nao katika fainali inayodhamiwa na Emirate Aluminium. Nyota hao ni pamoja na beki wa kazi ngumu na chafu Shomari Kapombe pamoja na kiungo wa kupekecha Pape Sakho. Kapombe aliweza…