
YANGA:LIGI NI NGUMU,TIMU ZOTE ZIMEJIPANGA
NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa ligi sio nyepesi kwa kuwa kila timu imejipanga kupata pointi tatu. Kwenye msimu wa 2021/22 mpaka sasa Yanga haijapoteza mchezo hata mmoja baada ya kucheza mechi 10 ikiwa imeshinda nane na kulazimisha sare mechi mbili. Mchezo wake uliopita ilikuwa mbele ya Biashara United ambapo ilishinda mabao 2-1…