KIUNGO HUYU KUSEPA MANCHESTER UNITED
KIUNGO wa Klabu ya Manchester United inayoshiriki Ligi Kuu England, Paul Pogba ataondoka bure ndani ya kikosi hicho msimu wa 2021/22 utakapomeguka kwa kuwa mabosi wa timu hiyo wamethibitisha kwamba hawatamuongezea dili jingine. Mwishoni mwa msimu huu Pogba mkataba wake utameguka na kuanzia Januari 2022 atakuwa huru kufanya mazungumzo na klabu nyingine ambayo inahitaji saini…