AZAM FC WAPINDUA MEZA MBELE YA KAGERA SUGAR

LICHA ya Kagera Sugar kuanza kufunga kupitia kwa Anuary Jabir dk ya 10 mbele ya Azam FC,walikwama kupata pointi tatu jumlajumla.

Ilikuwa katika Uwanja wa Azam Complex, Agosti 17, meza ilipinduliwa kupitia kwa Prince Dube aliyepachika bao la kwanza dk ya 17 na lile bao la ushindi kwa Azam FC lilifungwa na Tepsi Evance dk ya 58.

Mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa ni wa kwanza kwa timu zote mbili msimu wa 2022/23 ambao umeanza kwa kasi kubwa kwa timu zote kusaka ushindi.

Kiungo Tepsi ameweka wazi kuwa ulikuwa ni mchezo mgumu na wenye ushindani lakini wameweza kupata ushindi.

“Ninawashukuru viongozi kwa kuweza kuniamini na kunipa nafasi nina amini kwamba tutazidi kupambana ili kupata matokeo kwenye mechi zetu zijazo,”,.

Jabir wa Kagera Sugar amesema kuwa mchezo huo umekwisha wao wakiwa wamepoteza hesabu zao ni mchezo ujao dhidi ya Simba.

“Tumepoteza mchezo sasa tunaangalia mchezo wetu ujao wa ligi ambao ni dhidi ya Simba,”.