ATAKAYEVAA KITAMBAA KWA WASHIKA BUNDUKI NI ODE

KLABU ya Arsenal imemtangaza rasmi Martin Odegaard kuwa ni nahodha mpya kuelekea msimu mpya wa 2022/2023.

Arsenal ilimsajili mchezaji huyo kutoka timu ya Real Madrid kwa mkopo kabla ya kukamilisha dili la kumsajili moja kwa moja kwa ada ya Paundi milioni 30 kufuatia kufanya vizuri ndani ya kikosi hicho cha washika mtutu wa London.

Hivyo nyota huyo ana kazi ya kuvaa kitambaa kwa washika bunduki hao ambao wanatamani ligi ianze waone kasi yao mpya chini ya Kocha Mkuu, Mikel Arteta.

 Kabla ya Odegaard kitambaa cha unahodha kilikuwa kikivaliwa na Granit Xhaka huku akisaidiwa mara kadhaa na kinda wa timu hiyo Bukayo Saka.

Tayari Arsenal ipo katika maandalizi ya msimu mpya huku ikitarajiwa kufungua pazia la Ligi Kuu nchini Uingereza ambapo inatarajiwa kucheza dhidi ya Crystal Palace siku ya Ijumaa ya Agosti 5, 2022.