>

AZAM KUKIWASHA LEO MISRI KWA MARA YA KWANZA

AZAM FC leo wanatarajia kucheza mchezo wa kirafiki wakiwa nchini Misri ambao ni maalumu kwa ajili ya benchi la ufundi kutazama namna vijana wao walivyoweza kuwa imara.

Huu unakuwa ni mchezo wa kwanza kwa Azam FC ambayo inatarajiwa kutumia siku 20 ikiwa Misri kwa maandalizi ya msimu mpya.

Kocha Mkuu wa Azam FC,Abdi Hamid Moallin amesema kuwa ambacho anakitazama si matokeo bali muunganiko wa wachezaji pamoja na uwezo wa kuweza kuwatumia kwenye mechi za ushindani.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa leo Julai 27 nchini Misri ambapo timu hiyo imeweka kambi itakuwa dhidi ya Klabu ya Wadi Degla.

 “Tunahitaji kucheza mechi za kirafiki ili kuwa imara na kwenye mechi yetu hatuangalii matokeo hilo sio kipaumbele wetu bali ambacho tunaangalia ni namna ambavyo itakuwa kwa wachezaji kile ambacho watakifanya.

“Wamekuwa kwenye mazoezi mazuri na magumu na wanaonekana kufurahia hilo ni jambo jema lakini bado kuna wachezaji wapya na wale ambao walikuwepo hivyo ni lazima kuweza kuona muunganiko wao,”.