PABLO YUPO DAR TAYARI KUINOA SIMBA

PABLO Franco, Kocha Mkuu wa Simba leo Novemba 10 amewasili Dar kwa ajili ya kujiunga na timu hiyo inayowania kutetea taji la Ligi Kuu Bara.

Kocha huyo amekuja kuchukua mikoba ya Didier Gomes ambaye alibwaga manyanga kutokana na kushindwa kutimiza lengo la kwanza la timu hiyo la kutinga hatua ya makundi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kupoteza kwa kufungwa mabao 3-1 dhidi ya Jwaneg Galax kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa kuliwavuruga mabosi wa Simba jambo ambalo Gomes aliamua kuwajibika kwa kuwa yeye alikuwa ni kocha mkuu.

Pablo amesaini dili la miaka miwili kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo ambapo mshahara wake na bonasi yake kwenye kila hatua atakayopiga ni kubwa.

Amekuja kuungana na Hitimana Thiery pamoja na Seleman Matola ambao wapo kwenye benchi la ufundi la Simba.