>

KIM POULSEN:HAITAKUWA KAZI RAHISI MBELE YA DR CONGO

KIM Poulsen, Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars amesema kuwa mchezo wa kesho dhidi ya DR Congo haitakuwa kazi rahisi kwa wachezaji lakini ni muhimu kupambana ili kupata matokeo chanya.

Kesho, Stars ina kibarua kikubwa cha kusaka ushindi mbele ya DR Congo kwenye mchezo wa kuwania Kufuzu Kombe la Dunia wakiwa na kumbukumbu ya kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa DR Congo.

Poulsen amesema kuwa amewaambia wachezaji wana kazi kubwa ya kufanya na wasikifikiri kwamba kuongoza kundi J kazi imekwisha kwa kuwa wana mtihani mwingine mzito wa kufanya kusaka pointi tatu.

“Kazi haijaisha na kwa kuwa tuna mchezo mbele ya DR Congo tunajua kwamba haitakuwa kazi rahisi hilo lipo wazi na wachezaji wanajua hivyo tutanaamini kwamba tutapambana kusaka ushindi kwa kuwa hakuna kingine ambacho kinahitajika.

“Jambo la kufurahisha ni kwamba mashabiki watakuwepo na tunapata ushirikiano mkubwa kutoka serikalini na hilo linatupa nguvu ya kuona kwamba tunapaswa kusaka ushindi hivyo mashabiki waendelee kuwa pamoja nasi tunaamini kwamba tutafanya vizuri,” amesema.

Kwenye kundi J, Stars inaongoza kundi ikiwa na pointi saba ikiwa sawa na Benin tofauti ikiwa kwenye idadi ya mabao ya kufunga na kufungana huku DR Congo ikiwa nafasi ya tatu na ile ya nne ipo mikononi mwa Madagascar.

Baada ya mchezo wa kesho, Stars itakuwa na kazi yakusaka pointi tatu nyingine mbele ya Madagascar.