UWANJA wa London mambo yalikuwa magumu kwa Liverpool kwenye mchezo wa Ligi Kuu England baada ya kutulizwa kwa kufungwa mabao 3-2 dhidi ya Westham United.
Atajilaumu Alisson Ramses Becker ambaye alijifunga dakika ya nne katika harakati za kuokoa kona kisha Pablo Fornals alipachika kamba ya pili dakika ya 67 na msumari wa ushindi ulipachikwa na Kurt Zouma dakika ya 74 kwa West Ham United.
Yale ya Liverpool yalipachikwa na Alexander-Arnold dakika ya 41 na la pili lilipachikwa na Divock Orogi dakika ya 83 jambo lililofanya Jurgen Klopp kushuhudia timu yake ikichapwa kwa mara ya kwanza msimu huu tangu Aprili.
Kocha Mkuu wa West Ham United, David Moyes amesema kuwa ni ushindi mkubwa na mzuri mbele ya timu kubwa huku Klopp wa Liverpool akibainisha kuwa bao la kwanza ilikuwa ni faulo ya wazi kabisa ila imekataliwa na watu wanaweza kusema anatafuta huruma jambo ambalo sio kweli.