BREAKING:MORRISON ASIMAMISHWA SIMBA

TAARIFA rasmi kutoka ndani ya Simba zimeeleza kuwa mchezaji wao Bernard Morrison amesimamishwa ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Pablo Franco.

Kupitia ukurasa rasmi wa Instagram wa Simba umeeleza kuwa umempa mapumziko ya muda mpaka mwisho wa msimu mchezaji huyo.

Taarifa imeeleza kuwa wamefikia hapo ili kumpa muda wa Morrison kushughulikia mambo yake binafsikwa makubaliano ya pande zote mbili.

Pia Simba imeeleza kuwa inamshukuru Morrison kwa mchango wake ambao ameweza kuutoa ndani ya Simba kwa miaka miwili ambayo ameitumikia timu hiyo.