KAZE:TUTAPAMBANA KUPATA POINTI TATU

CEDRICK Kaze,Kocha Msaidizi wa Yanga amesema kuwa kwa mechi ambazo zimebaki watapambana kupata pointi tatu muhimu kwa kuwa walizikosa zile za Simba.

Kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Aprili 30,2022 Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Yanga 0-0 Simba hivyo watani hao wa jadi waligawana pointi tatu.

Akizungumza na Saleh Jembe,Kaze amesema kuwa wana kazi kubwa ya kufanya kwenye mechi zijazo kupata ushindi.

“Kuna kazi kubwa ya kusaka ushindi kwenye mechi zetu ambazo zimebaki na haitakuwa kazi nyepesi kwani kila timu inahitaji ushindi kwa namna moja ama nyingine.

“Ushindani ambao upo ni mkubwa kwani kila mechi ni muhimu kwetu kushinda na hilo wachezaji wanalitambua nasi pia tunahitaji ushindi,”amesema.

Yanga ina kazi ya kusaka ushindi kwenye mchezo dhidi ya Ruvu Shooting mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma kesho Mei 4,2022.