REAL MADRID WATWAA TAJI LA 35

KLABU ya Real Madrid imetwaa taji la 35 la La Liga baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Espanyol wakiwa nyumbani.

Taji hilo pia linamfanya Kocha Mkuu Ancelotti raia wa Italia kuwa kocha wa kwanza kutwaa mataji makubwa Ulaya katika ligi 5 bora.

Aliweza kufanya hivyo England, Hispania, Ujerumani,Italia na Ufaransa.

Nahodha Benzema alitupia bao alitokea benchi ilikuwa dk 81 huku mabao mengine yakifungwa na Rodrygo dk 33 na 43 na Marco Asensio alitupia dk 55.

Uwanja wa Santiago Bernabeu uliwafanya wakusanye pointi 81 na Sevilla ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 64 zote zimecheza mechi 34.

Espanyol ipo nafasi ya 13 na pointi 39 kibindoni.