Home International SALAH ATWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA

SALAH ATWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA

MSHAMBULIAJI wa Klabu ya Liverpool raia wa Misri Mohamed Salah ametwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Ligi Kuu ya Uingereza kutoka kwa Shirikisho la Waaandishi wa Habari za Michezo nchini humo.

Salah mwenye umri wa miaka 29 amekuwa na msimu mzuri akiwa na klabu yake ya Liverpool baada ya kufanikiwa kufumania nyavu mara 22 na kutoa pasi 13 za mabao kwenye jumla ya michezo 32 ya Ligi Kuu nchini Uingereza huku akiwa na jumla ya mabao 30 na pasi 14 za mabao katika michezo 45 aliyoshiriki kwenye mashindano yote.

Mshambuliaji huyo anatwaa tuzo hiyo ambayo msimu uliopita ilichukuliwa na beki wa kati wa Manchester City Ruben Dias lakini pia Salah ndiye kinara wa mabao wa Ligi Kuu ya Uingereza akiwa na jumla ya mabao 22, mabao matano zaidi ya Son Heung-Min wa Tottenham Hotspurs na Cristiano Ronaldo wa Manchester United.

Previous articleMANCHESTER CITY WAPIGA 4G LEEDS UNITED
Next articleREAL MADRID WATWAA TAJI LA 35