NYOTA wa kikosi cha Manchester United amesema kuwa anaamini bado miaka minne au mitano kwenye soka na pia ana furaha kufanya kazi hiyo anayoipenda.
Kwa sasa bado anakipiga ndani ya Manchester United akiwa ni staa anayetajwa kuwa mshambuliaji bora wa muda wote.
Nyota huyo kibindoni ana tuzo tano za Ballon d’Or na msimu huu tayari ametupia mabao 15 katika mechi 28.
Ronaldo amesema hayo kutokana na kukosolewa hivi karibuni kutokana na kushindwa kuwa na mchango kwenye timu yake.
“Ni ngumu kusema lolote kwa sasa, ila ninaamini bado nitakuwa ndani ya soka kwa muda wa miaka minne ama mitano mbele nipo kuipambania Man United,”