HATARI YA MORRISON KIMATAIFA IPO HIVI

MTUKUTU Bernard Morrison mzee wa kuchetua kiungo mshambuliaji wa Simba ana wastani wa kuwa na hatari kila baada ya dakika 57 akiwa uwanjani kwenye mechi za kimataifa.

Simba ikiwa imecheza mechi nneBM ametumia dakika 172 na ametupia mabao matatu katika mechi tatu ambazo amecheza.

Alianza kuonyesha makeke mbele ya Red Arrows alitumia dakika 90 alitupia mabao mawili moja ilikuwa ni kwa pigo huru dakika ya 16 na alipachika bao la pili dakika ya 77 kwa pasi ya Mohamed Hussein.

Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Mkapa ilikuwa ni Novemba 28,2021 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 3-0 Red Arrows

Katika mchezo wa marudio uliochezwa Uwanja wa Taifa wa Heroes, Zambia ilikuwa ni Desemba 5,2021 Morrison alitumia dakika 56.

Kutokana na tatizo la utovu wa nidhamu Morrison alisimamishwa na alikosekana kwenye mchezo dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast na Simba ilishinda mabao 3-1.

Aliibuka kwenye mchezo dhidi ya USGN ya Niger alitumia dakika 26 na alipachika bao dakika ya 83 kwa pasi ya Shomari Kapombe ilikuwa ni Februari 20,2022.