VIJANA wa Jurgen Klopp waliamua kushusha mvua za mabao mwa wapinzani wao Leeds United kwenye mchezo wa Ligi Kuu England kwa kusepa na pointi tatu mazima.
Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Anfield ulisoma Liverpool 6-0 Leeds United.
Ni Mohamed Salah alitupia mawili na yote kwa penalti dakika ya 15 na 35 huku Joel Matip yeye akitupia bao moja dk ya 30, Sadio Mane pia alitupia mawili dk ya 80 na 90.
Jioni kabisa wakati Leeds United wakiamini kazi imeisha beki kisiki Virgil van Dijk alitupia bao dk 90+3.
Sasa Liverpool imefikisha pointi 60 tofauti ya pointi 3 na vinara Manchester City wenye pointi 63 kibindoni na wote wamecheza mechi 26.