Mchezaji wa Simba, Aziz Ki, amewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi uwanjani na kuwaunga mkono katika kipindi chote cha mchezo ili kuwapa hamasa ya kupambana na kutafuta ushindi.
Aziz Ki amesema sapoti ya mashabiki ni muhimu kwa timu, hasa wakati mchezo unapokuwa mgumu, akieleza kuwa wanahitaji mashabiki wawatie moyo na kuinua morali ya wachezaji hadi dakika za mwisho.
“Tunawahitaji mashabiki wawe nyuma ya timu katika kipindi chote cha mchezo. Wakati mambo yanapokuwa magumu, watutie moyo na kuinua morali yetu. Wakati mambo yanapokwenda vizuri, waendelee kutusukuma ili tupate bao la kwanza na kuongeza bao la pili,” amesema Aziz Ki.
Aidha, amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi na kujaza uwanja ili kutengeneza mazingira yatakayowapa wachezaji hamasa ya kupambana hadi mwisho wa mchezo.
Akizungumzia maandalizi ya timu kuelekea kuanza kwa mashindano hayo, Aziz Ki amesema wachezaji wamekuwa wakisubiri kwa hamu wakati huo na wamefanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya kuanza kampeni yao kwa ushindi.
Ameeleza kuwa kuanza mashindano wakiwa nyumbani ni faida kubwa ambayo wanapaswa kuitumia vizuri kwa kuhakikisha wanapata matokeo mazuri mbele ya mashabiki wao.
“Wote tumekuwa tukiusubiri kwa hamu wakati huu. Tumefanya maandalizi ya kutosha na tuko tayari kutoa kila kitu uwanjani ili kuanza kampeni yetu ya mashindano haya kwa ushindi,” amesema.
Ameongeza kuwa timu ina wajibu wa kutumia vizuri faida ya kucheza nyumbani kwa kupambana kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo huo wa kwanza.
Aziz Ki amehitimisha kwa kutoa wito kwa mashabiki kujitokeza kwa wingi na kuendelea kuwa sehemu muhimu ya safari ya timu katika mashindano hayo.