Kocha Mkuu wa Manchester Unite, Ole Gunnar Solskjaer anatarajiwa kubaki na kuendelea kuinoa timu hiyo licha ya mwendelezo wa matokeo mabovu hususani ya bao 5-0 aliyapata juzi baada ya kupigwa na Liverpool, Sky Sports Italia imethibitisha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Klabu ya Manchester, Richard Arnold jana alivunja appointment zote za vikao vya wageni ili kukutana na Mmiliki wa Klabu hiyo, Joel Glazer kwa ajili ya kujadili hatima ya Solskjaer.
Licha ya tetesi za kutimuliwa kwake huku Antonio Conte akihusishwa,imedaiwa kuwa Uongozi unatarajia kujikita zaidi katika kuboresha hali iliyopo kuliko kumtimua kocha huyo.
Katika mazungumzo yake, baada ya mchezo wa siku ya Jumapili, Ole Gunner alinukuliwa akisema wamepambana kwa pamoja kwa muda mrefu lakini wanakaribia kushindwa huku akisisitiza kipigo cha 5-0 kilikuwa ni kibaya zaidi katika kazi yake.