Hatua ya 16 Bora ya Kombe la Dunia 2026 imekamilika rasmi usiku wa kuamkia leo baada ya timu nane kufuzu hatua ya robo fainali.
Mabingwa wa dunia wa mwaka 2018, Ufaransa, watakutana na Morocco katika mchezo utakaochezwa Julai 9 katika Uwanja wa Boston, Huku Morocco ikihitaji kulipiza kisasi baada ya kutolewa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Dunia la mwaka 2022.
Siku inayofuata, Julai 10, Hispania itachuana na Ubelgiji katika Uwanja wa Los Angeles kwenye mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na kiwango kizuri kilichoonyeshwa na mataifa hayo katika michuano hiyo.
Mnamo Julai 11, Norway itashuka dimbani dhidi ya England katika mchezo wa robo fainali utakaochezwa katika Uwanja wa Miami, huku timu zote zikisaka nafasi ya kuandika historia mpya kwenye Kombe la Dunia.

Katika mchezo mwingine wa robo fainali utakaochezwa siku hiyo hiyo, mabingwa wa kombe la dunia mwaka 2022, Argentina itavaana na Uswisi katika Uwanja wa Kansas City kutafuta nafasi ya kutinga hatua ya nusu fainali.
Hatua ya robo fainali inatarajiwa kushuhudia ushindani mkubwa huku timu zote nane zikisaka tiketi nne za kuelekea hatua ya nusu fainali ya Kombe la Dunia 2026.

JULAI 09 | Saa 23:00
France
Morocco
JULAI 10 | Saa 22:00
Spain
Belgium
JULAI 12 | Saa 00:00
Norway
England
JULAI 12 | Saa 04:00
Argentina
Switzerland
Je, ni timu zipi zitafuzu hatua ya Nusu Fainali?