Argentina 3-2 Misri, FIFA Kombe la Dunia 2026

Argentina 3-2 Misri, FIFA Kombe la Dunia 2026 ni matokeo ambayo yamekuwa pigo kwa timu ya Misri kutoka Afrika iliyoanza kwa kuongoza katika 67 za mchezo huku V.A.R ikifuta bao moja kwa upande wao.

Magoli ya Misri yamefungwa na Yasser Ibrahim dakika ya 15 na Mostafa Ziko dakika ya 67. Walikwenda mapumziko wakiwa wanaongoza.

Nyota Messi alikosa mkwaju wa penati kwenye mchezo huo kipindi cha kwanza mara baada ya mlinda mlango wa Misri kuokoa penati hiyo.

Argentina wamefunga kupitia Critian Romero dakika ya 79, Lionel Messi dakika ya 83 na Enzo Fernandez dakika ya 90+3.

Hawa ni mabingwa watetezi wanakata tiketi kutinga hatua ya robo fainali wakiwaondoa wawakilishi kutoka Afrika ambao walikuwa kwenye nafasi nzuri kushinda mchezo wa leo Julai 7,2026.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, itakuwa mezani Julai 10,2026 jiandae kuipata.