Nado afungukia ishu ya kuikamia Simba SC

KIUNGO mshambuliaji wa Azam FC, Idd Nado amefunguka kuhusu kudaiwa kuwa anaikamia sana Simba SC kwenye mechi ambazo wanakutana.

Nado amekuwa kwenye ubora msimu wa 2025/26 ambapo timu hiyo imemaliza kwenye msimamo ikiwa nafasi ya 3 baada ya kukusanya jumla ya pointi 64.

Dhidi ya Simba SC kwenye mechi mbili walipata ushindi mchezo mmoja na sare moja ambapo katika mchezo walioshinda 2-0 Nado alifunga bao moja.

Kiungo huyo amesema amekuwa akiulizwa kuhusu kuikamia Simba SC akiwa katika kikosi cha Azam FC mara kwa mara.

“Nimekuwa nikiulizwa kuhusu kuikamia sana Simba SC nakucheza katika ubora kwenye mechi ambazo tunakutana. Ukweli ni kwamba nilipokuwa Mbeya City nilikuwa naifunga sana Yanga SC wakasema huyu mtoto atakuwa ni Simba SC.

“Wakati huu nimekuwa nafanya vizur dhidi ya Simba SC wanasema huyu atakuwa Yanga SC, hili linaniumiza msimu ujao nikiwa Azam FC nitawajibu,”.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, itakuwa mezani Julai 10,2026 jiandae kuipata.