Mchezo wa hatua ya 16 bora, Portugal vs Spain FIFA Kombe la Dunia 2026 umewaachia maumivu timu Ronaldo. Mikel Merino aliingia akiwa ni mchezaji wa akiba na kufunga bao la ushindi kwa Hispania, wakishinda Ureno ya Cristiano Ronaldo 1-0 jijini Dallas Jumatatu usiku na kukatisha safari ya gwiji huyo katika Kombe la Dunia huku Hispania ikijihakikishia nafasi ya robo fainali ya 2026.
Ilikuwa ni bao lililojengwa kwa ustadi mkubwa wa timu ya Hispania, kupitia pasi safi dakika ya 90. Ferran Torres alitoa pasi murua ya kupenya safu ya ulinzi, ikampata kiungo wa Arsenal, Merino, ambaye alitimiza mbio zake kwa wakati sahihi ndani ya boksi la Ureno. Merino alimalizia kwa utulivu akimpita kipa Diogo Costa dakika chache tu baada ya kuingia, na kuhakikisha bao lake ndilo pekee katika Derby ya Iberia.
Wakati Hispania walitumia vyema nafasi yao ya kuamua matokeo, ilikuwa mwisho wa majonzi kwa Ureno na pia kuaga kwa heshima moja ya nguli wakubwa wa soka.Mshambuliaji mkongwe Cristiano Ronaldo alihitimisha kile kinachotarajiwa kuwa Kombe lake la Dunia la mwisho, akimaliza kampeni ya 2026 akiwa na mabao matatu.
Kocha Roberto Martínez alikuwa na matumaini kwamba CR7 angeleta tofauti katika kile kilichoweza kuwa mechi yake ya mwisho kwenye jukwaa kubwa zaidi la soka.Nyota huyo mwenye umri wa miaka 41 alipewa nafasi ya kuanza katika mechi zote tano za Ureno huko Amerika Kaskazini, lakini pambano la Jumatatu dhidi ya wapinzani wao waliowashinda mwaka 2025 kutwaa taji la Nations League lilikuwa changamoto kubwa na halikuwa mchezo wa kufurahisha kwake.
…
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, itakuwa mezani Julai 10,2026 jiandae kuipata.