Paredi la ubingwa Yanga SC laacha historia

Paredi la ubingwa Yanga SC Julai 4,2026 limeacha historia kutokana na burudani kutolewa kutoka kwa wasanii mbalimbali huku Dj Zee akitoa burudani.

Ni Mohamed Hussen Zimbwe Jr beki bora wa muda wote ndani ya NBC Premier League alikuwa na jukumu la kuwapandisha wachezaji wa timu hiyo ambao walikuwepo Bongo.

Miongoni mwa wachezaji hao ni Allan Okello kiungo ambaye amekuwa katika ubora msimu wa 2025/26 akisajiliwa katika usajili wa dirisha dogo.

Mbal na Okello, Pacome ambaye yupo hospitali akiendelea na matibabu ni miongoni mwa wachezaji ambao wameombewa dua na mashabiki wa Yanga SC na familia ya michezo ili arejee katika ubora.

Yanga SC imetwaa taji la ligi mara 5 mfululizo na mdhamini mkuu wa timu hiyo ni kampuni ya SportPesa.

Hii ni historia kubwa kwa Yanga SC kudumu kwenye ubora kwa kutwaa mataji na kufanya paredi ambalo lilikuwa na mashabiki wengi.

Paredi hilo lilipita mtaa wa Msimbazi ambapo hapo watani zao wa jadi Simba SC mashabiki walikuwa wamekusanyika kwa kutazama mchezo wa fainali vs Azam FC, CRDB Federation Cup.

Simba SC walipata ushindi wa bao 1-0 na leo wamefanya paredi la ubingwa wakipita pia mitaa ya Jangwani.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, itakuwa mezani Julai 10,2026 jiandae kuipata.