Azam FC vs Yanga SC CRDB Federation Cup

Azam FC vs Yanga SC CRDB Federation Cup ni mchezo unaofuata kwenye hatua ya nusu fainali Juni 21, 2026 Uwanja wa CCM Kirumba.

Mabingwa watetezi wa taji hili ni Yanga SC ambao wanapambana kutetea taji hilo huku Azam FC wakiwa na hesabu yakutinga fainali.

Mshindi wa mchezo wa nusu fainali ya pili atakutana na Simba SC kwenye mchezo wa fainali kusaka bingwa mpya 2026.

Simba SC imekata tiketi Juni 20, 2026 kwa ushindi wa mabao 4-0 Coastal Union katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

Florent Ibenge, Kocha Mkuu wa Azam FC amesema wanatambua umuhimu wa mchezo huo watapambana kupata matokeo mazuri.

“Tunatambua umuhimu wa mchezo na tupo tayari kwa ajili ya ushindani kikubwa ni kuona tunapata matokeo chanya,”.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.