VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga SC msimu wa 2025/26 wamekusanya mtaji mkubwa kwenye magoli yakufunga huku wakiruhusu magoli machache.
Timu hiyo inapambania taji ililotwaa msimu wa 2024/25 ambapo kwa sasa mshindani wake namba moja ni Simba SC anafuatia Azam FC ambaye yupo nafasi ya tatu.
Yanga SC baada ya mechi 25 safu ya ushambuliaji imefunga magoli 58 ikiwa ni timu namba moja kufunga magoli mengi inafuatiwa na Simba SC yenye magoli 45.
Kweye upande wa magoli yakufungwa, Yanga SC imefungwa machache kwenye ligi ambayo ni 9 sawa na Azam FC huku Simba SC ikiwa imefungwa magoli 10 baada ya zote zimecheza jumla ya mechi 25.
Ikiwa watagongana pointi uwezekano mkubwa wa ubingwa upo kwenye mikono ya Yanga SC kutokana na tofauti ya magoli jambo ambalo linaongeza ushindani ndani ya ligi.
Kwenye pointi mpaka sasa ni tofauti ya pointi 2 dhidi ya timu iliyo nafasi ya pili na pointi 8 dhidi ya timu iliyo nafasi ya 3 yenye pointi 52.
…
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.