Yanga SC 3-1 Namungo FC NBC Premier League

Yanga SC 3- 1 Namungo FC, NBC Premier League, Mei 25, 2026, Uwanja wa KMC Complex pointi tatu zikiwa ni mali ya wenyeji wakibeba zote jumlajumla.

Magoli ya Yanga SC yamefungwa na Duke Abuya dakika ya 26 na mawili yamefungwa na Allan Okello dakika ya 84 ikiwa ni goli lake 11.

Goli pekee la Namungo FC limefungwa na Hassan Kabunda dakika ya 39. Ushindi huo unaifanya Yanga SC kurejea nafasi ya kwanza kwenye msimamo ikifikisha jumla ya pointi 60 baada ya mechi 25, Simba SC nafasi ya pili na pointi 58.

Okello ametwaa tuzo ya Man of the Match akiwa ni mkali kwenye kucheka na nyavu amefikisha jumla ya magoli 11.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.