JKT Tanzania yagawana alama na Fountain Gate kwenye mchezo wa NBC Premier League leo Mei 21, 2026 kwa kufungana magoli 2-2.
Fountain Gate ya Issa Mbulizi ilianza kupata magoli ya kuongoza mapema kipindi cha kwanza ni kazi ya Juma Abushiri dakika ya 3 na Ismail Kader dakika ya 45.
Mpaka dakika 45 za mwanzo zinakamilika ubao ulikuwa unasoma JKT Tanzania 0-2 Fountain Gate hivyo kipindi cha pili wenyeji walipindua meza.
Wenyeji walifunga goli la kwanza dakika ya 54 kupitia Saleh Karabaka na Paul Peter aliweka mzani sawa dakika ya 86 wakigawana pointi mojamoja.