MCHEZO wa NBC Premier League umekamilika ubao wa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga umesoma Coastal Union 1-2 Simba SC.
Ni Maabad Maabad alifungua ukurasa wa magoli dakika ya 9 kwa shuti kali huku Libasse Gueye aliweka usawa dakika ya 37 na goli la ushindi limefungwa na Anicent Oura dakika ya 44 akitumia pasi ya Clatous Chama.
Ushindi huo unamfanya mnyama kufikisha pointi 55 anakuwa nafasi ya kwanza baada ya mechi 24 nafasi ya pili ni Yanga SC yenye pointi 54 baada ya mechi 23.
Yanga SC kesho Mei 22, 2026 anakibarua cha kusaka pointi 3 muhimu dhidi ya Singida Black Stars mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa KMC Complex.
…
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.