CRDB Cup ratiba ya robo fainali hii hapa

CRDB Cup ni hatua ya robo fainali ambapo timu zinatarajiwa kushuka uwanjani kusaka ushindi kutinga hatua ya nusu fainali.

Haya ni mashindano mengine makubwa Bongo ambapo ni hatua ya mtoano mpaka fainali ukishinda unasonga mbele ukifungwa umeumaliza mwendo.

Katika mashindano haya ambayo yapo hatua ya robo fainali mabingwa watetezi ni Yanga SC watakuwa kazini Mei 16 kusaka nafasi kutinga hatua ya nusu fainali.

Mei 16, 2026 ni Coastal Union vs Singida Black Stars, saa 10:00 jioni,  JKT Tanzania vs Yanga SC, saa 12:30, Jumapili Mei 17 zitapigwa mechi mbili kali pia.

Mashujaa FC vs Azam FC saa 10:00 jioni, Simba SC vs TRA United, saa 12:30, washindi kwenye kila mechi watasonga mbele hatua ya nusu fainali.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.