Waziri Mkuu Aeleza Mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita Kwenye Michezo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amepongezwa kwa uongozi wake mahiri, dira pana na dhamira ya dhati ya kuwekeza katika sekta ya michezo ambapo chini ya Serikali ya Awamu ya Sita, sekta hiyo imepiga hatua kubwa ambazo leo zinashuhudiwa kwa fahari, kuongezeka hamasa, ushindani na mafanikio ya timu na wanamichezo mbalimbali katika anga za kitaifa na kimataifa.

Akizungumza katika usiku wa tuzo za Bazara la Michezo la Taifa (BMT) zilizotolewa kwa wanamichezo na timu zilizofanya vizuri mwaka 2025, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba ambaye alikuwa mgeni rasmi amesema katika kipindi kifupi yameshuhudiwa mafanikio makubwa, yakiwamo kuanzishwa kwa Mfuko wa Maendeleo ya Michezo unaopata 5% ya mapato ya michezo ya kubashiri ambao umewezesha timu hizo na wanamichezo kushiriki mashindano mengi zaidi na kwa ubora wa juu.

“Aidha, bajeti ya wizara imeongezeka kutoka shilingi bilioni 35.4 mwaka 2022/2023 hadi bilioni 525.3 mwaka 2026/2027 ongezeko kubwa kuwahi kutokea. Programu za hamasa kama Goli la Mama na Knock Out ya Mama zimeongeza ari na matokeo mazuri ya timu zetu, ikiwemo vilabu vya Tanzania kufika hatua ya fainali ya kombe la Afrika kwa mara ya kwanza katika historia amesisitiza, Dkt. Mwigulu.

Ameongeza kuwa kila mmoja ameona mafanikio ya wanamichezo wakiwamo Alfonce Simbu pamoja na mabondia wakubwa Ibrahim Class; timu za Taifa Stars, timu ya Kriketi, na Futsal zikishiriki mashindano ya dunia pamoja na uwekezaji mkubwa katika viwanja vya michezo vya Benjamin Mkapa, Aman Zanzibar, Arusha, Dodoma