Simba SC 1-0 JKT Tanzania ni matokeo rasmi kwenye mchezo wa leo NBC Premier League, Mei 6, 2026, Uwanja wa Meja Jeneral Isahmuyo.
Goli la ushindi limefungwa na kiungo mshambuliaji Clatous Chama dakika ya 54 limetosha kuipa timu hiyo pointi tatu muhimu.
Mara baada ya mchezo kukamilika kiungo Chama amechaguliwa kuwa Man of the Match kutokana na kiwango ambacho amekionyesha.
Msimu wa 2025/26, Simba SC imevuna pointi 6 mbele ya JKT Tanzania kwa kushinda nje ndani, mzunguko wa kwanza ilikuwa JKT Tanzania 1-2 Simba SC.
Matokeo haya yanaifanya Simba SC kurejea nafasi ya pili ikiwa na pointi 46 huku tofauti na vinara Yanga SC ikibaki palepale pointi 5.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.