Walioipa ushindi Simba SC vs JKT Tanzania watakosekana mazima

WACHEZAJI walioipa ushindi Simba SC vs JKT Tanzania mzunguko wa kwanza leo watakosekana mazima kutokana na sababu mbalimbali.

Ikumbukwe kwamba katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Meja Jeneral Isahmuyo baada ya dakika 90 ubao ulisoma JKT Tanzania 1-2 Simba SC.

Magoli ya Simba SC yalifungwa na Wilson Nangu na Jonathan Sowah. Mastaa hawa wawili leo hawapo kwenye mpango wa kikosi kazi cha Kocha Mkuu, Steve Barker.

Nangu yupo nje kutokana na kutokuwa fiti huku Sowah yeye ni matatizo ya kinidhamu ambapo adhabu yake ilikuwa ni kwenda kufanya mazoezi na timu ya vijana U 20.

Leo Simba SC iliyo nafasi ya tatu kwenye msimamo itakabiliana na JKT Tanzania iliyo nafasi ya 5 kwenye msimamo saa 12:15 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Mbali na Sowah, Anicet Oura, Mousa Camara na Hamza Jr nao wapo nje kutokana na kutokuwa fiti.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.