Yanga SC vs Simba SC, fainali Muungano Cup inatarajiwa kuchezwa kesho Aprili 29, 2026 Uwanja wa New Amaan Complex.
Mechi hii itachezwa kuanzia saa 2:15 usiku kwa wababe wawili kukutana uwanjani kusaka bingwa wa Muungano Cup 2026.
Ikumbukwe kwamba mabingwa watetezi wa taji hilo ni Yanga SC inayonolewa na Kocha Mkuu, Pedro Goncalves.
Simba SC chini ya Kocha Mkuu, Steve Berkar 2025 hawakushiriki Muungano Cup kutokana na ratiba yao katika mashindano ya CAF walipotinga hatua ya fainali Cofideration Cup.
Mpaka sasa kinara wa utupiaji magoli ni Prince Dube akiwa ametupia magoli matatu anafuatiwa na Seleman Mwalimu wa Simba SC mwenye magoli mawili.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.