Yanga SC vs Simba SC, Muungano Cup fainali

Yanga SC vs Simba SC ni Dabi ya Kariakoo, Kombe la Muungano Cup kwa wababe hawa kupambana kusaka taji.

Mchezo huu unatarajiwa kuchezwa kesho 29/4/2026 Jumatano, Uwanja wa New Amaan Complex Zanzibar, kuanzia majira ya saa 2:15 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Yanga SC wanaingia katika mchezo huu kama mabingwa watetezi, huku watani zao Simba SC Wakisaka kuivua ubingwa Yanga SC.

Ikumbukwe kwamba Yanga SC wamepata ushindi kwenye mechi zote ambazo wamecheza Muungano Cup kwa kufunga jumla ya magoli 6 na wakiruhusu goli moja dhidi ya Azam FC.

Katika mechi hizo zote mbili Man of The Match alitoka Yanga SC, mchezo waliopata ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya Muembe Makumbi ni Shekhan Khamis na mchezo wa magoli 2-1 dhidi ya Azam FC ni Duke Abuya alitwaa tuzo hiyo.

Wanakutana na Simba SC iliyopata ushindi wa jumla ya magoli manne kwenye mechi mbili ndani ya dakika 180, Simba SC 1-0 Mafunzo na Simba SC 3-0 Mlandege FC.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.