Mabingwa watetezi wa Muungano Cup Yanga SC wametinga hatua ya fainali kwa ushindi wa magoli 2-1 Azam FC.
Ni Prince Dube alifungua ukurasa wa magoli dakika ya 9 kwa pasi ya Allen Okelo na kamba ya pili mali ya Maxi Nzengeli kwa pasi ya Dube dakika ya 24.
Goli pekee la Azam FC limefungwa na Fei Toto dakika ya 78 likiwa ni lakufutia machozi. Matajiri wa Dar walitinga hatua hiyo kwa ushindi wamagoli 2-0 dhidi ya KVZ magoli yote yakifungwa na Ngita Jean aliyechaguliwa kuwa Man Of The Match.
Mchezaji bora hatua ya nusu fainali alichaguliwa Duke Abuya amezawadiwa milioni moja na Chuo cha Afya Zanzibar School of Health na Fuetes Mendoza wa Azam FC alizawadiwa laki 5 kwa kuchaguliwa kuwa mchezaji aliyeonyedha mchezo wa kiungwana zaidi, (Best Fair Play).
Yanga SC wanasubiri mshindi wa mchezo wa leo kati ya Simba SC vs Mlandege FC unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa New Amaan Complex saa 2:15 usiku.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.