Yanga SC vs Azam FC ni leo Muungano Cup

Yanga SC vs Azam FC ni leo Aprili 25, 2026 kwenye hatua ya nusu fainali Muungano Cup, Uwanja wa New Amaan Complex.

Hii ni Nusu Fainali ya kwanza, ya mashindano ya Muungano Cup 2026, ambao unajulikana kama ‘Dar es Salaam Derby’.

Ikumbukwe kwamba Yanga SC imefika hatua hii baada ya kuifunga Muembe Makumbi City 4-0 katika Robo Fainali, huku Azam FC ikiichapa KVZ FC mabao 2-0.

Kocha Mkuu wa Azam FC, Florent Ibenge amesema kuwa wapo tayari kwa mchezo mkubwa wanatambua utakuwa na ushindani ndani ya uwanja.

“Tupo tayari kwa ajili ya mchezo mkubwa na tunatambua kwamba utakuwa bora, kikubwa ni utayari na wachezaji na kufanya vizuri mchezo wetu,”.

Pedro Goncalves, Kocha Mkuu wa Yanga SC ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa kila mchezo malengo ni kupata matokeo mazuri.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.