Manchester City imekwea rasmi kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza kufuatia ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Burnley katika dimba la Turf Moor.
Bao pekee la mchezo lilifungwa mapema dakika ya tano na mshambuliaji nyota Erling Haaland, akiendeleza ubora wake msimu huu na kuipa City alama tatu muhimu ugenini.
Ushindi huo unaifanya Manchester City kufikisha alama 70 baada ya michezo 33, sawa kabisa na Arsenal waliopo nafasi ya pili. Timu hizi mbili pia zina uwiano sawa wa mabao (+33), lakini City wanaongoza jedwali kutokana na kufunga mabao mengi zaidi (66 dhidi ya 63 za Arsenal).

Katika upande mwingine, matokeo hayo yameihakikishia Burnley kushuka daraja rasmi na sasa wataungana na timu za EFL Championship msimu ujao, baada ya kushindwa kujinasua kutoka eneo la hatari.
Wakati huo huo, mchezo mwingine wa ligi ulishuhudia AFC Bournemouth wakilazimishwa sare ya mabao 2-2 na Leeds United, matokeo ambayo yanaendelea kufanya vita ya kujiokoa dhidi ya kushuka daraja kuwa ngumu zaidi.
Kwa sasa, mbio za ubingwa wa EPL zimezidi kuwa kali huku Manchester City na Arsenal wakitofautiana kwa vigezo vidogo tu, jambo linaloashiria hatima ya taji hilo kuamuliwa katika mechi chache zilizosalia msimu huu.
Mechi kuna mechi zilizobaki kwa Arsenal na Manchester City katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza (wakati wakiwa wamecheza mechi 33):