Barcelona vs Celta Vigo Patashika Kubwa Camp Nou Usiku wa Leo

Patashika nguo kuchanika Leo tarehe 22 Aprili 2026, saa 10:30 usiku kwa saa za Afrika Mashariki, uwanja wa Spotify Camp Nou huko Barcelona utakuwa jukwaa la pambano la kusisimua la La Liga kati ya Barcelona na Celta Vigo.

Barcelona wanaingia kwenye mechi hii wakiwa kileleni mwa msimamo wa La Liga wakiwa na pointi 76 baada ya kucheza mechi 30, wakifuatiwa kwa karibu na Real Madrid wenye pointi 69.Kwa upande mwingine, Celta Vigo wanashika nafasi ya sita kwenye msimamo wakiwa na pointi 44, wakiwa katika harakati za kuhakikisha nafasi ya kushiriki michuano ya Ulaya msimu ujao .

Barcelona ina rekodi nzuri ya kuvutia nyumbani msimu huu, wakiwa wameshinda mechi tisa kati ya kumi za nyumbani katika mechi kumi za mwisho. Barcelona wanaongoza kwa mabao 80 wakifungwa 29 tu, wakiwa na rekodi bora ya kushambulia na moja ya ulinzi bora katika ligi. Wachezaji kama Lamine Yamal wamekuwa wakionyesha ubora wa hali ya juu msimu huu, na uchezaji wao wa ubunifu unatarajiwa kuwa muhimu katika kuvunja safu ya ulinzi ya Celta Vigo.

Upande wa Celta Vigo, timu hiyo inakabiliwa na changamoto kubwa ya kucheza ugenini dhidi ya timu yenye rekodi nzuri nyumbani. Celta wamefanikiwa kupata pointi 16 katika mechi zao kumi za ugenini, wakiwa na ushindi nne, sare nne, na kupoteza mbili. Timu hiyo inategemea sana mashambulizi ya haraka lakini kufanya hivyo dhidi ya Barcelona kwenye uwanja wao ni changamoto kubwa. Ulinzi wao wa pembeni utahitaji kuwa makini sana kukabiliana na wachezaji wepesi wa Barcelona kama Rashford na Ferran Torres.

Ingia kwenye kasi ya kujishindia pesa kwenye michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi

Mechi hii ina umuhimu mkubwa kwa timu zote mbili kwa sababu tofauti. Kwa Barcelona, ushindi utawapa pointi muhimu za kujiimarisha kileleni mwa msimamo, hasa wakijua kwamba Real Madrid wanawafuatia kwa karibu kwa tofauti ya pointi saba pekee . Kwa mechi sita tu zimesalia hadi mwisho wa ligi, kila pointi ni muhimu katika harakati za kutwaa ubingwa.

Kwa Celta Vigo, wanahitaji kudumisha nafasi yao ya sita inayowapa tiketi ya kushiriki michuano ya Ulaya, kwani Real Betis wana pointi 45 na wanawafuatia kwa karibu . Tofauti ya pointi tatu tu kati yao inamaanisha kuwa Celta hawawezi kumudu kupoteza pointi nyingi katika kipindi hiki cha mwisho cha ligi.

Katika michezo ya hivi karibuni, mechi zimekuwa za kuvutia na mabao mengi. Katika msimu huu, Barcelona waliwafunga Celta Vigo mabao 4-2 ugenini tarehe 9 Novemba 2025. Katika msimu uliopita, walishinda nyumbani kwa mabao 4-3. Takwimu hizi zinaonyesha kuwa licha ya ubora wa Barcelona, Celta wamekuwa wakifanikiwa kuwapa changamoto na hata kuwafunga mabao kadhaa katika michezo yao.

Kocha wa Celta, Giraldez Claudio, anajulikana kwa uwezo wake wa kuandaa timu zake kwa mbinu za kukabiliana na timu zenye nguvu. Hata hivyo, kukiwa na wachezaji wengi wa Barcelona walio na uwezo wa kuamua mchezo kwa wakati wowote, Celta watakuwa na kazi kubwa ya kuzuia mashambulizi ya Barcelona wakati wote wa mechi. Jisajili sasa