Simba , TRA United Zapigwa Faini Baada ya Stewards Kupigana Uwanjani

Klabu za Simba SC na TRA United zimetozwa faini ya Tsh. milioni tano kila moja kwa kosa la walinzi wa klabu hizo (Stewards) kupigana mara baada ya timu hizo kuwasili kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

Adhabu hiyo imetolewa leo Aprili 20, 2026 na kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Aprili 18, 2026 baada ya kupitia mwenendo na matukio mbalimbali ligi ambapo tukio hilo likitokea kabla ya mchezo baina ya timu hizo uliomalizika kwa sare tasa katika uwanja huo.