Bayern Munich Wahitaji Ushindi Leo Kutangaza Ubingwa wa Bundesliga

Klabu ya Bayern Munich inaweza kutangazwa Bingwa wa Ujerumani leo iwapo haitapoteza dhidi ya VfB Stuttgart katika Dimba la Allianz Arena.

Mabingwa hao watarajiwa wamepata nafuu baada ya mpinzani wao wa karibu, Borussia Dortmund, kupoteza kwa wiki ya pili mfululizo.

Dortmund ilifungwa bao la dakika za mwisho na TSG Hoffenheim kwa mabao 2-1. Kwa sasa, Dortmund ina alama 64 na hata ikishinda michezo yake yote minne iliyobaki, inaweza kufikia alama 76 ambazo tayari Bayern Munich inazo.

Hata hivyo, Bayern imepata pigo baada ya kuthibitisha kuwa mshambuliaji wake Serge Gnabry atakuwa nje ya uwanja kwa muda usiojulikana kutokana na majeraha ya misuli ya paja.

Kutokana na jeraha hilo, Gnabry atakosa mechi za nusu fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Paris Saint-Germain. Pia, uwezekano wake wa kushiriki kombe la Dunia uko mashakani, kwani majeraha ya aina hii huchukua muda mrefu kupona.

Msimu huu, Gnabry amecheza mechi 37 na kufunga mabao 10 akiwa na Bayern Munich.