Chelsea Wafikiria Kumuuza Alejandro Garnacho Baada ya Msimu Mgumu Stamford Bridge

 

Chelsea wanafikiria kumuweka sokoni winga wao Chelsea Alejandro Garnacho katika dirisha lijalo la majira ya joto, kufuatia msimu uliokuwa mgumu kwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 21 tangu aliposajiliwa kwa pauni milioni 40 akitokea Manchester United.

Garnacho, aliyesajiliwa siku ya mwisho ya dirisha la usajili Septemba, ameanza mechi 21 kati ya 51 za Chelsea, na amefunga mabao manane yote mashindano mbalimbali, lakini ni bao moja tu lililofungwa kwenye Ligi Kuu ya England.

Taarifa zinaeleza kuwa kocha wa Chelsea Liam Rosenior ana mashaka kuhusu mchango wa mchezaji huyo, huku akimpa nafasi ndogo zaidi kwenye kikosi cha kwanza tangu alipochukua majukumu Januari 6. Badala yake, nafasi ya winga wa kushoto imekuwa ikichukuliwa zaidi na Pedro Neto, huku usajili mpya Jamie Gittens akiwa nje kutokana na majeraha.

Kabla ya kujiunga na Chelsea, Garnacho alionekana kuwa na shauku kubwa ya kuhamia klabuni hapo, huku wakala wake hata wakifanya mazungumzo Stamford Bridge miezi kadhaa kabla ya uhamisho kukamilika.

Hata hivyo, maisha yake Chelsea na hata nyuma yake United yamekuwa na misuguano ya nidhamu na maamuzi ya makocha. Alishutumiwa baada ya mechi ya mwisho ya Europa League dhidi ya Tottenham Hotspur, na pia alikosa kikosi dhidi ya Aston Villa kutokana na mtazamo wa kocha.

Garnacho pia aliwahi kuomba radhi baada ya kuondoka uwanjani kabla ya muda katika mechi dhidi ya Ipswich Town, tukio lililoibua mjadala kuhusu nidhamu yake ndani ya timu.

Sasa mustakabali wake Stamford Bridge uko mashakani, huku Chelsea wakipima uwezekano wa kumuuza endapo ofa nzuri itawasilishwa msimu ujao.