Mashujaa FC 0-0 Azam FC mchezo umekamilika kwa wababe kugawana pointi mojamoja katika Uwanja wa Lake, Tanganyika mwisho wa reli Kigoma.
Matokeo haya yanaifanya Azam FC kusalia nafasi ya pili wakiongeza pointi moja kibindoni leo Machi 19,2026.
Ni pointi 29 wanafikisha Azam FC baada ya mechi 15 NBC Premier League wakiwa hawajapoteza mchezo mpaka sasa kwenye ligi.
Mashujaa FC wanafikisha jumla ya pointi 19 nafasi ya 11 kwenye msimamo baada ya mechi 17 msimu wa 202526.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.