Soko la Michezo ya Kubahatisha La Stake Lapata Nguvu Kutoka Expanse Studios

Sekta ya michezo ya kubahatisha duniani imepata habari njema baada ya Expanse Studios kutangaza rasmi ushirikiano mpya na jukwaa kubwa la ubashiri la kimataifa, Stake. Hatua hii inakuja baada ya mafanikio makubwa ya kampuni hiyo katika kushirikiana na wadau mbalimbali wa tasnia, akiwemo Meridianbet. Ushirikiano huu unatarajiwa kuleta msisimko mpya kwa wachezaji huku ukipanua upatikanaji wa michezo bunifu katika soko la kimataifa.

Kwa miaka kadhaa sasa, Expanse Studios imekuwa ikitambulika kama kinara wa ubunifu katika uandaaji wa michezo ya kubahatisha yenye ubora wa hali ya juu. Michezo kama Super Heli, Wild Icy Fruits, na VASO Psycho imekuwa gumzo miongoni mwa wabashiri duniani kutokana na muundo wake wa kisasa na burudani ya kipekee wanayopata watu kila wakicheza. Sasa kupitia Stake, michezo hii maarufu itawafikia wachezaji wengi zaidi duniani.

Kampuni ya Expanse Studios ipo chini ya mwavuli wa Meridian Holdings Inc., kundi kubwa linalomiliki na kusimamia chapa kadhaa zenye mafanikio katika tasnia ya michezo na burudani. Miongoni mwa kampuni hizo ni Meridianbet Group inayofanya kazi katika masoko mengi duniani, RKings nchini Uingereza, Mexplay nchini Mexico pamoja na Classics for a Cause inayotekeleza shughuli zake nchini Australia.

Akizungumzia makubaliano hayo, Mtendaji Mkuu wa Expanse Studios, Damjan Stamenkovic, alisema kampuni hiyo inajivunia kuanza safari mpya na Stake, chapa inayoheshimika sana katika ulimwengu wa michezo ya kubahatisha. Alieleza kuwa kupitia miundombinu ya Hub88, ushirikiano huo utaongeza wigo wa upatikanaji wa michezo ya Expanse na kuwafikia wachezaji wengi zaidi katika majukwaa ya kimataifa.

Ikiwa na zaidi ya washirika 1,300 duniani pamoja na mkusanyiko wa zaidi ya michezo 70 ya kipekee, Expanse Studios inaendelea kujenga historia mpya katika tasnia ya michezo ya kubahatisha. Ushirikiano na Stake unaonesha dhamira ya kampuni hiyo ya kuendelea kupanua mipaka ya ubunifu, kuwapa wachezaji burudani ya kiwango cha juu, na kuimarisha uwepo wake katika majukwaa makubwa ya kimataifa.