Tanzania Prisons vs Yanga SC kupigwa Tabora?

Tanzania Prisons vs Yanga SC kupigwa Tabora? Ni swali ambalo linaulizwa ni baada ya wenyeji kubainisha kuwa watakuwa Tabora kwenye mechi zinazofuata.

Wapinzani hawa wawili wanatarajiwa kukutana Machi 12,2026 kwenye msako wa pointi tatu muhimu ndani ya uwanja.

Ipo wazi kwamba Prisons wamekuwa wakitumia Uwanja wa Sokoine kwa mechi za nyumbani uliopo Mbeya kutokana na kufungiwa na Shirikisho la Soka Tanzania wamechagua Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora.

Taarifa zinaeleza kuwa tayari Prisons wameshaweka kambi Tabora kwa maandalizi ya mwisho wa mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Wageni Yanga SC ni vinara wa ligi na wametoka kupata ushindi mkubwa wa magoli 7-1 dhidi ya Polisi Tanzania mchezo wa CRDB Federation Cup.

Prisons imetoka kupoteza katika mchezo wa CRDB Federation Cup kwa kufungwa goli 1-0 dhidi ya TMA Stars ambayo inatarajiwa kukutana na Yanga SC hatua ya 16 bora.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.