Home Sports SIMBA YAIVUTIA KASI DAR CITY

SIMBA YAIVUTIA KASI DAR CITY

KIKOSI cha Simba leo kimefanya mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Dar City.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Januari 30 na mshindi atasonga hatua ya 16 bora

Katika mchezo wa hatua ya 32 bora yule atakayepoteza mchezo safari yake inafika ukingoni jumlajumla.

Ikumbukwe kwamba Simba ni mabingwa watetezi wa Kombe la Shirikisho ambapo waliweza kushinda katika mchezo wa fainali mbele ya Yanga.

Fainali hiyo ilipigwa katika Uwanja wa Lake Tanganyika,mwisho wa reli Kigoma.

Miongoni mwa mastaa wa Simba ambao walikuwepo mazoezini ni pamoja na Meddie Kagere, Erasto Nyoni, John Bocco na Chris Mugalu.

Previous articleSIMBA QUEENS KAZINI LEO DHIDI YA MLANDIZI QUEENS
Next articleSIMBA QUEENS YAPETA MBELE YA MLANDIZI QUEENS