UWANJA wa Bunju Complex, Simba Queens imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mlandizi Queens.
Oppa Clement ametupia mawili na moja alitupia kwa penalti na bao jingine lilitupiwa na Laiya Barakat.
Pongezi kubwa kwa kipa namba moja wa Mlandizi Queens ambaye alikuea ni mikono mia.
Noaely Marakuti alikuwa imara langoni ndani ya dakika 90 owa kuweza kuokoa hatari za washambuliaji wa Simba Queens.
Kwa upande wa Simba Queens, Joel Bukuru alikuwa ni nyota katika mchezo huo na mapigo yote huru yalikuwa miguuni mwake.